Ruka hadi maudhui
SAVIORINVENTORY SYSTEM

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Nahitaji intaneti kila wakati?

Hapana. Programu ya simu inafanya kazi bila intaneti: unauza na kurekodi matumizi kama kawaida, na mabadiliko yanatumwa intaneti ikirudi. Kwenye kompyuta unahitaji intaneti.

Majaribio ya bure yanafanyaje kazi?

Unajisajili na kupata siku 14 za kutumia huduma zote bure. Hakuna malipo yanayokatwa yenyewe. Ukipenda, unalipia kifurushi.

Nalipiaje?

Kwa pesa za simu: ombi la malipo kwenye simu yako, au namba ya malipo (control number) unayolipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au CRDB. Kifurushi kinawashwa malipo yakifika.

Nini kinatokea kifurushi kikiisha?

Taarifa zako zinabaki salama na unaweza kuziangalia. Huwezi kuongeza mauzo au matumizi mapya mpaka ulipie tena. Tunakukumbusha siku 7, 3 na 1 kabla.

Taarifa zangu ziko salama?

Ndiyo. Kila biashara inaona taarifa zake tu. Unaingia kwa namba ya simu na nenosiri, na tunatengeneza nakala za akiba (backup) za database.

Naweza kuongeza wafanyakazi?

Ndiyo. Mpe kila mfanyakazi jukumu: meneja, keshia, mtunza stoo, mhasibu au uzalishaji, au chagua ruhusa mwenyewe. Mmiliki pekee ndiye anaona faida na kulipia.

Inafanya kazi kwenye simu gani?

Simu za Android na iPhone, na pia kwenye kompyuta au tablet kupitia kivinjari (browser).

Nikisahau nenosiri?

Bonyeza "Umesahau nenosiri?" na upate nambari ya siri kwa SMS au barua pepe. Mmiliki pia anaweza kuweka nenosiri jipya kwa mfanyakazi.

Inafaa kwa biashara ya aina gani?

Maduka, wauzaji wa jumla, maduka ya dawa, vifaa vya ujenzi, migahawa, na wanaozalisha bidhaa kama mikate, juisi au sabuni.

Anza kuona faida yako leo

Jaribu SAVIOR bure kwa siku 14. Ukihitaji msaada wa kuanza, tupigie au tuandikie WhatsApp.

Anza bureIngia