Ruka hadi maudhui
SAVIORINVENTORY SYSTEM

Huduma za SAVIOR

Zana zote unazohitaji kuendesha biashara yako vizuri, bila kuwa mtaalamu wa kompyuta.

Mauzo na risiti

Uza kwa sekunde chache. Stoku inapungua yenyewe na kila risiti inapata namba yake (R00001, R00002...).

  • Punguzo kwa mteja
  • Bei ya kununulia inahifadhiwa ili faida iwe sahihi
  • Kufuta mauzo kunarudisha stoku

Bidhaa na stoku

Kila mabadiliko ya stoku yanarekodiwa: stoku ya mwanzo, manunuzi, mauzo, marekebisho na marejesho.

  • Nani, lini na kwa nini
  • Kiwango cha tahadhari kwa kila bidhaa
  • Tafuta na panga kwa makundi

Njia za malipo

Rekodi jinsi mteja alivyolipa, ili ujue pesa iko wapi.

  • Taslimu na benki
  • M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa
  • Mauzo ya mkopo (deni)

Matumizi

Kodi, mishahara, usafiri, umeme na maji, na mengine. Matumizi ya kila mwezi yanarekodiwa yenyewe.

  • Weka mara moja, mf. kodi TZS 150,000 kila tarehe 1
  • Tarehe zilizopita zinajazwa
  • Alama ya "Otomatiki"

Ripoti na faida

Mapato, gharama ya bidhaa zilizouzwa, faida ghafi, matumizi na faida halisi, kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.

  • Bidhaa zinazouzwa zaidi
  • Mauzo kwa njia ya malipo
  • Mauzo kwa siku au kwa mwezi

Wafanyakazi na majukumu

Ongeza wafanyakazi wako na uchague kila mmoja anaruhusiwa kufanya nini.

  • Meneja, keshia, mtunza stoo, mhasibu, uzalishaji
  • Mmiliki pekee anaona faida na kulipia
  • Kumbukumbu ya nani alifanya nini

Uzalishaji

Kwa wanaotengeneza bidhaa (mikate, juisi, sabuni...): weka mapishi, na malighafi zinapungua unapozalisha.

  • Mapishi ya kila bidhaa
  • Gharama ya kuzalisha
  • Stoku ya bidhaa iliyokamilika inaongezeka

Taarifa za haraka

SAVIOR inakukumbusha mambo muhimu bila wewe kuuliza.

  • Stoku ikipungua au kuisha
  • Muhtasari wa mauzo ya jana
  • Kumbusho kabla kifurushi hakijaisha

Inafanya kazi bila intaneti

Programu ya simu (Android na iPhone) inaendelea kufanya kazi bila mtandao, na inatuma mabadiliko intaneti ikirudi.

  • Inatuma mabadiliko tu, inaokoa bando
  • Hakuna kitu kinarekodiwa mara mbili
  • Pia kwenye kompyuta kupitia kivinjari

Usalama na nakala

Taarifa za kila biashara zimetengwa. Unaingia kwa namba ya simu na nenosiri.

  • Nakala za akiba (backup) za database
  • Umesahau nenosiri? Nambari kwa SMS au barua pepe
  • Kifurushi kikiisha bado unaona taarifa zako

Kiswahili na Kiingereza

Chagua lugha unayoipenda. Hali ya giza (dark mode) inafuata simu yako.

  • Kiswahili ndiyo lugha ya kwanza
  • Fedha kwa TZS
  • Inafaa kwa simu ndogo pia

Anza kuona faida yako leo

Jaribu SAVIOR bure kwa siku 14. Ukihitaji msaada wa kuanza, tupigie au tuandikie WhatsApp.

Anza bureIngia