Hujui faida halisi
Pesa inaingia na kutoka, lakini mwisho wa mwezi hujui kama umepata faida au hasara.
Kwa maduka, wauzaji wa jumla, migahawa na wazalishaji
Rekodi mauzo, matumizi na stoku kwa simu yako. SAVIOR inakuhesabia faida halisi, inakuonya stoku ikiisha, na inafanya kazi hata bila intaneti.
Unajisajili kwa namba ya simu tu. Hakuna malipo wakati wa majaribio.


Data ya duka la mfano
Pesa inaingia na kutoka, lakini mwisho wa mwezi hujui kama umepata faida au hasara.
Stoku inapungua bila maelezo, na huwezi kujua nani aliuza nini na lini.
Kumbukumbu za miezi mingi zinapotea pamoja na daftari moja.
Mteja anakuja kununua, lakini bidhaa imeisha na hukujua mapema.
Imetengenezwa kwa ajili ya biashara za Tanzania: Kiswahili, TZS na pesa za simu.
Uza kwa sekunde chache. Stoku inapungua yenyewe na kila risiti inapata namba yake (R00001, R00002...).
Kila mabadiliko ya stoku yanarekodiwa: stoku ya mwanzo, manunuzi, mauzo, marekebisho na marejesho.
Kodi, mishahara, usafiri, umeme na maji, na mengine. Matumizi ya kila mwezi yanarekodiwa yenyewe.
Mapato, gharama ya bidhaa zilizouzwa, faida ghafi, matumizi na faida halisi, kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.
Ongeza wafanyakazi wako na uchague kila mmoja anaruhusiwa kufanya nini.
Programu ya simu (Android na iPhone) inaendelea kufanya kazi bila mtandao, na inatuma mabadiliko intaneti ikirudi.
Fungua akaunti kwa namba yako ya simu na jina la biashara. Inachukua chini ya dakika moja.
Ongeza bidhaa, bei ya kununua na kuuza, na stoku uliyonayo sasa.
Rekodi kila mauzo na matumizi. SAVIOR inakuhesabia faida yenyewe.
Kifurushi kimoja chenye huduma zote. Chagua muda unaokufaa.
Hapana. Programu ya simu inafanya kazi bila intaneti: unauza na kurekodi matumizi kama kawaida, na mabadiliko yanatumwa intaneti ikirudi. Kwenye kompyuta unahitaji intaneti.
Unajisajili na kupata siku 14 za kutumia huduma zote bure. Hakuna malipo yanayokatwa yenyewe. Ukipenda, unalipia kifurushi.
Kwa pesa za simu: ombi la malipo kwenye simu yako, au namba ya malipo (control number) unayolipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au CRDB. Kifurushi kinawashwa malipo yakifika.
Taarifa zako zinabaki salama na unaweza kuziangalia. Huwezi kuongeza mauzo au matumizi mapya mpaka ulipie tena. Tunakukumbusha siku 7, 3 na 1 kabla.
Ndiyo. Kila biashara inaona taarifa zake tu. Unaingia kwa namba ya simu na nenosiri, na tunatengeneza nakala za akiba (backup) za database.
Jaribu SAVIOR bure kwa siku 14. Ukihitaji msaada wa kuanza, tupigie au tuandikie WhatsApp.