Ruka hadi maudhui
SAVIORINVENTORY SYSTEM

Kwa maduka, wauzaji wa jumla, migahawa na wazalishaji

Jua faida yako kila siku

Rekodi mauzo, matumizi na stoku kwa simu yako. SAVIOR inakuhesabia faida halisi, inakuonya stoku ikiisha, na inafanya kazi hata bila intaneti.

Unajisajili kwa namba ya simu tu. Hakuna malipo wakati wa majaribio.

Kurekodi mauzo mapya kwenye SAVIOR kwa kugusa bidhaa
Dashibodi ya SAVIOR kwenye simu: mauzo ya leo, mauzo ya siku 7 na bidhaa inayokaribia kuisha
M-Pesa, Mixx, Airtel Money
Inafanya kazi bila intaneti
Onyo stoku ikiisha

Data ya duka la mfano

Je, haya yanakutokea?

Hujui faida halisi

Pesa inaingia na kutoka, lakini mwisho wa mwezi hujui kama umepata faida au hasara.

Bidhaa zinapotea

Stoku inapungua bila maelezo, na huwezi kujua nani aliuza nini na lini.

Daftari linapotea au kuharibika

Kumbukumbu za miezi mingi zinapotea pamoja na daftari moja.

Bidhaa inaisha ghafla

Mteja anakuja kununua, lakini bidhaa imeisha na hukujua mapema.

Kila kitu cha biashara yako mahali pamoja

Imetengenezwa kwa ajili ya biashara za Tanzania: Kiswahili, TZS na pesa za simu.

Mauzo na risiti

Uza kwa sekunde chache. Stoku inapungua yenyewe na kila risiti inapata namba yake (R00001, R00002...).

Bidhaa na stoku

Kila mabadiliko ya stoku yanarekodiwa: stoku ya mwanzo, manunuzi, mauzo, marekebisho na marejesho.

Matumizi

Kodi, mishahara, usafiri, umeme na maji, na mengine. Matumizi ya kila mwezi yanarekodiwa yenyewe.

Ripoti na faida

Mapato, gharama ya bidhaa zilizouzwa, faida ghafi, matumizi na faida halisi, kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.

Wafanyakazi na majukumu

Ongeza wafanyakazi wako na uchague kila mmoja anaruhusiwa kufanya nini.

Inafanya kazi bila intaneti

Programu ya simu (Android na iPhone) inaendelea kufanya kazi bila mtandao, na inatuma mabadiliko intaneti ikirudi.

Anza kwa hatua 3

  1. 1

    Jisajili

    Fungua akaunti kwa namba yako ya simu na jina la biashara. Inachukua chini ya dakika moja.

  2. 2

    Weka bidhaa zako

    Ongeza bidhaa, bei ya kununua na kuuza, na stoku uliyonayo sasa.

  3. 3

    Anza kuuza

    Rekodi kila mauzo na matumizi. SAVIOR inakuhesabia faida yenyewe.

Bei rahisi na wazi

Kifurushi kimoja chenye huduma zote. Chagua muda unaokufaa.

Majaribio ya bure ya siku 14

Tumia huduma zote bure kwa siku 14. Hakuna malipo mpaka uamue kuendelea.

Miezi 3

TZS47,000kwa mwezi

Jumla TZS 141,000 kwa siku 90

Okoa 6%
Anza bure
Thamani bora

Mwaka 1

TZS45,000kwa mwezi

Jumla TZS 540,000 kwa siku 365

Okoa 10%
Anza bure

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Nahitaji intaneti kila wakati?

Hapana. Programu ya simu inafanya kazi bila intaneti: unauza na kurekodi matumizi kama kawaida, na mabadiliko yanatumwa intaneti ikirudi. Kwenye kompyuta unahitaji intaneti.

Majaribio ya bure yanafanyaje kazi?

Unajisajili na kupata siku 14 za kutumia huduma zote bure. Hakuna malipo yanayokatwa yenyewe. Ukipenda, unalipia kifurushi.

Nalipiaje?

Kwa pesa za simu: ombi la malipo kwenye simu yako, au namba ya malipo (control number) unayolipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au CRDB. Kifurushi kinawashwa malipo yakifika.

Nini kinatokea kifurushi kikiisha?

Taarifa zako zinabaki salama na unaweza kuziangalia. Huwezi kuongeza mauzo au matumizi mapya mpaka ulipie tena. Tunakukumbusha siku 7, 3 na 1 kabla.

Taarifa zangu ziko salama?

Ndiyo. Kila biashara inaona taarifa zake tu. Unaingia kwa namba ya simu na nenosiri, na tunatengeneza nakala za akiba (backup) za database.

Anza kuona faida yako leo

Jaribu SAVIOR bure kwa siku 14. Ukihitaji msaada wa kuanza, tupigie au tuandikie WhatsApp.

Anza bureIngia